Matthew 28:18-20

18 aYesu akawajia na kusema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 19 bKwa sababu hii, enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, 20 cnanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika mimi niko pamoja nanyi siku zote, hadi mwisho wa nyakati.”

Copyright information for SwhNEN